Hongera Zitto,ni wakati wa kuweka makaratasi pembeni sasa haha
Nukuu
Mmoja wa watu waliokuwa wakishuhudia Zitto akitumia kifaa hicho kupitia luninga alisikika akisema.......
.........SPIKA atauliza Zitto hivi hako kakidude ni ka nini kako kama ka kompyuta?? hehehe
Mwingine nae akasema.....Hiyo itatoa usikivu wa wabunge wengine maana watakuwa wanashangaa ipad
Na mwingine.........Hivi kanuni za bunge zinahurusu kweli hichi kifaa? au spika hana muongozo! au anaogopa ataumbuka?
....hahaaaaa yaani spika anaweza kumfuta ubunge Zitto kwa kutumia chombo cha kiintelijensia bungeni...hahahaaaa hivi hii hawajaitolea muongozo kweli
........Kwa miaka ijayo matumizi ya kompyuta yawe ni sifa mojawapo ya mgombea ubunge. Sio ufundi wa kudai posho na siasa ya majukwaani.
...............I can imagine, wasira with all those makaratasi yesterday sijui atakuwa ana feel vipi?
Wasifu: Osama bin Laden
Siku ambayo ndege zilizotekwa nyara ziligonga majengo ya World Trade Centre na makao ya wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ni vitendo vilivyombadilisha Osama bin Laden kutoka mtu mdogo asiyejulikana na kumfanya kuwa mojawapo watu wanaotambulikana sana duniani.
Bofya SIKILIZA WASIFU WAKE
Bin Laden aliwahi kunukuliwa akisema: "Kile ambacho Marekani inakionja hivi leo ni kitu kidogo sana ikilinganishwa na kile ambacho tumekuwa tukikipata katika miongo kadhaa. Taifa letu limekabiliwa na hali hii ya kudhalilishwa na kudharaualiwa kwa zaidi ya miaka 80. Wanawe wanauwawa, damu yao inamwagwa, maeneo yake matakatifu yanahujumiwa na hayatawaliwi kwa mujibu wa amri zake Mwenyezi Mungu."
Osama bin Laden alizaliwa mwaka 1957 katika familia yenye utajiri mkubwa. Baba yake alianzisha kampuni kubwa ya ujenzi katika Saudi Arabia. Akiwa ni miongoni mwa ndugu 18 wa kiume, Osama aliwahi kufanya kazi katika biashara hiyo ya familia. Maisha yake yalianza kubadilika alipokuwa kijana pale Muungano wa Sovieti ulipoivamia Afghanistan.
Alipokwenda Aghanistan, Osama alikuwa kijana sana ambaye alitaka kujijengea umaarufu, katikati ya vita vitakatifu. Osama bin Laden alikaa kwa kipindi cha takriban miaka 10 nchini Afghanistan, na kuanzisha fungamano na wanaharakati wa siasa kali za kiislamu kote duniani.
Na baada ya majeshi yaliyovunjika moyo ya Sovieti kuondoka Afghanistan mnamo mwaka 1989. Osama bin Laden alirejea nyumbani Saudi Arabia. Mwaka mmoja baadaye alijitolea kumpa msaada wa kijeshi mfalme Fahad wakati Iraq ilipoivamia nchi jirani ya Kuwait. Lakini Osama alipatwa na mshtuko mkubwa pale Mfalme Fahad alipokataa toleo lake na badala yake kuigeukia Marekani.
Osama alinyaganywa uraia wa Saudi na akarejea Afghanistan ambayo wakati huo ikitawaliwa na Wataliban ambao alikubaliana nao kuhusu tafsiri ya uislamu.
Mnamo mwaka 1998 aliwahimiza waislamu wawauwe Wamarekani mkiwemo raia popote pale watakapowapata, kukafuatiwa mashambulio kadhaa ikiwa ni pamoja na dhidi ya balozi za Marekani katika Kenya na Tanzania na manowari ya USS Cole katika mwambao wa Yemen. Halafu shambulio la September 11, 2001.
Rais Bush alikunukuliwa kusema: "Sijui kama tutampata kesho au mwezi ujao au mwaka ujao. Lakini hapana shaka tutampata tu."
Ingawa Waislamu wengi walilaani vifo vya watu katika miji ya New York na Washington, Osama bin Laden alichukuliwa na wengi kuwa ni shujaa, aliyetetea haki za Wapalestina na kupinga nguvu za Marekani.
Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama bin Laden anaaminika kuacha watoto 17.
Senegal waandamana kupinga mgao wa umeme
Maandamano yamezuka katika mji mkuu wa Senegal, Dakar na katika jiji la kusini la Mbour kutokana na ukosefu wa umeme. Jijini Dakar, majengo kadhaa ya serikali yalichomwa moto, zikiwemo ofisi za shirika la umeme la serikali - Senelec.
Majeshi ya usalama katika mji wa Mbour yalipiga mabomu ya machozi kutawanya maelfu ya waandamanaji.
Tatizo la ukataji umeme, ambao umedumu kwa saa 48 katika maeneo kadhaa, limekuja wiki moja tu baada ya kutokea maandamano dhidi ya rais.
"Mamia ya vijana walivamia ofisi za Senelec na kuzichoma moto," amesema mkazi mmmoja wa Dakar, Ismail Diop akikaririwa na Reuters.
Chupa zilizovunjwa, mabaki ya majengo na matairi yaliyochomwa moto vimetapakaa mitaani, amesema mkazi huyo.
Miaka mingi
Mjini Mbour, karibu kilomita 80 kusini mashariki mwa Dakar, ofisi za shirika la umeme pia zilishambuliwa. watu walioshuhudia walisema ofisi za Senelec zilivunjwa na magari yaliyoegeshwa nje kushambuliwa pia.Senelec imeshindwa kutoa huduma ya umeme ya kuridhisha kwa miaka mingi.
Wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano mjini Dakar, yaliyotokana na pendekezo la rais Abdoulaye Wade kutaka kubadilisha katiba.
Maandamano hayo yalikuwa ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana katika kipindi cha miaka 11 ya utawala wa Bw Wade.
Gharama za maisha
Rais huyo alitaka kupunguza kiwango cha asilimia kinachohitajia kushinda urais kutoka asilimia 50 hadi 25 ili kuepuka duru ya pili katika uchaguzi.Wakosoaji wamesema marekebisho hayo ya katiba yamelenga kuhakikisha Rais Wade, ambaye ana umri wa miaka 85, anachaguliwa tena mwakani.
Bw Wade alingia madarakani katika uchaguzi wa kidemokrasia, lakini sasa anakabiliwa na ongezeko la hasira kutoka kwa wananchi kutokana na matatizo ya umeme ya kila siku na kupanda kwa gharama za maisha.
" DADA ZETU TUKISHINDWA KUWAHESHIMU MTATULAUMU?"
INABIDI KUKEMEA BIASHARA HII HARAMU.
Dada huyu ambaye hakutaka kutaja jina jina lake alikutwa maeneo ya flani akifanya biashara ya ngono bila kujali afya yake wala serekali yake kua biashara hiyo ni haramu. | |
LISHE BORA INAHITAJIKA KWA WAATHIRIKA WA HIV/AIDS.
"KWELI HAYA MAMBO YAMEHALALISHWA?"
Yaani bila kujali kama wana watoto au wadogo zao au hata watu waliowazidi umri wanthubutu kufanya mambo haya waziwazi hata kama ni kwa kificho lakini nchi na dini haviruhusu. Au wajihalalishia peke yao? KWANINI TUWATESE WANYAMA WANAOTUSAIDIA KATIKA SHUGHULI ZETU ZA KILA SIKU? HUU NI USAFIRI AU USAFIRI KAFIRI? 131 wadakwa kwa kulianzisha Mwanza.. nani alikuwa na shotgun na kudungua watatu?Polisi wasema wanamsakaPolisi mkoani Mwanza limesema limewakamata watu 131 kwa tuhuma za kuhusika na vurugu za wamachinga zilizosababisha kizaazaa kikubwa jana mjini mwanza. katika vurumai hizo, mali ziliporwa, ziliteketezwa kwa moto na kuharibiwa vibaya kama pichani inavyoonekana. Pia katika patashika hilo wapo watu waliojeruhiwa kwa risasi za moto.Watu waliojeruhiwa na kulazwa hospitali za Sekou Toure na Bugando ni Omari Abdallah, Juma Machumu (yupo mahututi- Bugando), Calvin Jeremiah, Brayen Pastori, Kulwa John (amepigwa risasi kichwani na yupo mahututi pia), Medard Benard na Dotto Thomas (amepigwa risasi). Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, na Kamishna Mwandamizi wa jeshi hilo, Simon Nyakoro Sirro, aliwaambia waandishi wa habari leo ofisini kwake kwamba, watu 131 waliokamatwa wanafanyiwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani. Mbali na watuhumiwa hao kutiwa mbaroni, polisi imesema risasi zilizotumika kuwapiga watu watatu ambao wanahali mbaya ni za bunduki aina ya Shotgun, na kwamba kwa sasa wapo kwenye uchunguzi wa kina kubaini na nani alitumia bunduki hiyo. "Kwa sasa tupo kwenye uchunguzi kubaini nani alitumia bunduki ama risasi za aina hii. Kimsingi bila nguvu kubwa tuliyoitumia mambo yangeliharibika zaidi...na mambo yakiharibika na mimi nitakuwa nimeharibikiwa", alisema RPC Sirro. Katika vurugu hizo baadhi ya majengo ya maduka ya wafanyabiashara yaliharibiwa kwa kupigwa mawe, likiwemo duka la Zara Solar mali ya Mohamed Papia jirani na msikiti wa Ijumaa barabara ya Nyerere, duka la Dubai Bazaar, Msikiti wa Jay Swaminarayan, Lake Printers lililopo barabara ya Kenyatta ambapo magari mawili yalichomwa moto na mengine kuvunjwa vioo Magari yaliyoharibiwa kwa kuvunjwa vioo ambayo ni mali ya mfanyabishara Mukesh Karia, ni T330 BHW, T943ANZ, T616 AHW na gari moja la kubebea wagonjwa namba hazikupatikana. DADA YETU AMELEWA NA MADAWA YAS KULEVYA NA HAPO ALIPO YUKO HOI
|