MADOIDO

MATANGAZO.

ADV

AURORA MARQUEE STYLE.

MICHEZO

                                   Mrisho Ngasa mchezaji toka Tanzania akiwa majaribioni kwenye timu yake inayotaka kumsajili ili awe anchezea timu hiyo wakati timu yake hiyo ilipokula kichapo cha mabao 7-0.   Tusiseme Ngassa hana bahati ila tumuombee afanikiwe ili aitangaze vyema nchi yetu ya Tanzania katika medani ya soka. Kirukaafrika, na Afrika Yetu inamuombea mafaniko mema katikamajaribio yake.                                                                                                                                                      




HII NDIYO MICHEZO YA AFRIKA NZIMA.
                                                                                                                                                                
Michezo ya Afrika Nzima (pia huitwa Michezo ya Afrika au Michezo ya Pan Afrika) ni tukio la michezo mbalimbali ya mataifa ya Afrika linalofanyika kila miaka minne, linaloandaliwa na Muungano wa Kamati za Kitaifa za Olimpiki za Afrika (ANOCA). Mataifa yote yanayoshiriki lazima yawe yanatoka katika bara la Afrika.
Makala ya kwanza yalifanyika mwaka wa 1965 katika mji wa Brazzaville, nchini Kongo. Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) ilitoa utambulisho rasmi kwa tukio hili kama tukio la bara la michezo mbalimbali, pamoja na michezo ya Pan American na Michezo ya bara Asia.

[hariri] Historia

Mwanzilishi wa Olimpiki ya kisasa Pierre de Coubertin alianzisha michezo ya Pan African mapema mwaka wa 1920. Mamlaka ya kikoloni yaliyokuwa yanatawala Afrika wakati huo yalikuwa yanahofia wazo hilo, yakishuku kuwa umoja wa Waafrika kupitia njia ya mchezo kungesababaisha Waafrika kudai uhuru wao.
Majaribio yalifanywa ili kuandaa michezo hiyo Algiers nchini Algeria na Alexandria,nchini Misri miaka ya 1925 na 1928 mtawalia, lakini licha ya maandalizi kabambe yaliyofanywa na waratibu, juhudi hizo zilitumbukia nyongo. Mwanachama wa kwanza kutoka Afrika wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, mwanariadha wa masafa mafupi aliyezaliwa nchini Ugiriki mwenye uraia wa Misri,Angelo Bolanaki, alichangia fedha kujengwe uwanja, lakini michezo haikufanyika hadi baada ya miongo mingine mitatu.
Katika miaka ya mapema ya sitini, nchi za Afrika zilizokuwa zinazungumza Kifaransa zilipanga Michezo ya Urafiki. Michezo hii ilipangwa na Madagascar (1960) na kisha Côte d'Ivoire (1961). Michezo ya tatu ilipangwa kufanyika nchini Senegal mwaka wa 1963. Kabla ya micheza hiyo kukamilika, Mawaziri wa Vijana na Mchezo wa Kiafrika walikutana Paris mwaka wa 1962, na kwa sababu chache za nchi zilizokuwa zinazungumza Kiingereza zilikuwa tayari zinashiriki, wao wakaipa Michezo hiyo jina la Michezo ya Pan Africa. Michezo hii ilipewa utambulisho rasmi na IOC kuwa katika kiwango sawa na michezo mingine ya kibara kama vile michezo ya bara Asia na Michezo ya Pan America.
Mnamo Julai mwaka wa 1965, makala ya kwanza yalifanyika Brazzaville, nchini Congo, sasa ikijulikana kama michezo ya All-Africa. Kutoka mataifa 30, idadi ya wanariadha karibu 2500 walishiriki. Misri ilishikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya medali.
Katika mwaka wa 1966, Kamati Kuu ya Michezo katika Afrika (SCSA) ilipangwa mjini Bamako; inasimamia michezo ya All-Africa. Makala ya pili yalituzwa nchi ya Mali katika mwaka wa 1969, lakini mapinduzi ya kijeshi yalilazimisha kufutiliwa mbali kwa Michezo hiyo. Lagos, Nigeria ilijitolea kuwa mwenyeji wa michezo hii mwaka wa 1971. Hatimaye michezo hiyo ilifanyika mwaka wa 1973 kutokana na Vita vya Biafra, ambavyo vilikuwa vimeisha karibuni nchini Nigeria.
Katika mwaka wa 1977, makala ya 3 ya michezo hii yalikuwa yamepangwa kufanyika nchini Algeria, lakini kutokana na sababu za kiufundi, yaliahirishwa kwa muda wa mwaka moja na yalifanyika mwaka wa 1978. Kuendeleza mtindo huu, makala yaliyofuata yalipangwa kufanyika nchini Kenya mwaka wa 1983, lakini yalisukumwa hadi mwaka wa 1985 na hatimaye yalifanyika mjini Nairobi mwaka wa 1987.
Mtindo wa Olimpiki wa miaka minne haujakosa kufuatwa tangu, na michezo hii imepangwa Cairo, Harare, Johannesburg, na Lagos. Katika mwaka wa 2007, Algiers kwa mara nyingine tena ilikuwa mwenyeji wa michezo na kuwa ya kwanza kurudia uwenyeji wa michezo hii. Lusaka nchini Zambia imejiondoa (mnamo Desemba 2008) kama mwenyeji wa makala yajayo ya michezo hii mwaka wa 2011.

 Miji wenyeji wa michezo hii

OrodhaMwakaJijiNchiTareheNchi yenye medali nyingi
11965BrazzavilleBendera ya Jamhuri ya Kongo Congo-BrazzavilleJulai 18 - Julai 25, 1965Bendera ya United Arab Republic United Arab Republic
--1969BamakoBendera ya Mali MaliUlikatizwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi
21973LagosBendera ya Nigeria NigeriaJanuari 7 - Januari 18, 1973Bendera ya Misri Egypt
31978AlgiersBendera ya Algeria AlgeriaJulai 13 - Julai 28, 1978Bendera ya Tunisia Tunisia
41987NairobiBendera ya Kenya Kenya1 Agosti - 12 Agosti, 1987Bendera ya Misri Egypt
51991CairoBendera ya Misri EgyptSeptemba 20 - Oktoba 1, 1991Bendera ya Misri Egypt
61995HarareBendera ya Zimbabwe Zimbabwe13 Septemba - 23 Septemba, 1995Bendera ya Afrika Kusini South Africa
71999JohannesburgBendera ya Afrika Kusini South Africa10 Septemba - 19 Septemba, 1999Bendera ya Afrika Kusini South Africa
82003AbujaBendera ya Nigeria Nigeria5 Oktoba - 17 Oktoba, 2003Bendera ya Nigeria Nigeria
92007AlgiersBendera ya Algeria AlgeriaJulai 11 - Julai 23, 2007Bendera ya Misri Egypt
102011MaputoBendera ya Msumbiji MozambiqueJulai 15 - Julai 27, 2011
Mji utakao kuwa mwenyeji wa makala ya 2015 ya michezo hii utaamuliwa hivi karibuni. Accra, Ghana na Kenya zimetajwa kama zenye uwezekano wa kuwa wenyeji.

 Orodha ya medali

Orodha inayofuata inaonyesha medali zilizohesabiwa katika makala yote ya michezo hii.

NafasiNchiDhahabuFedhaShaba-JumlaMwaka wa
medali ya kwanza
[1]Kigezo:EGY43132832010791965
2Bendera ya Nigeria Nigeria3032772568361965
3Kigezo:RSA1981741375091995
4Kigezo:ALG1321521894731965
5Kigezo:TUN123[85]1333621965
6Bendera ya Kenya Kenya90971042911965
7Kigezo:SEN4040731531965
8Kigezo:GHA2638641281965
9Kigezo:ETH232934861965
10Kigezo:CMR2042811431965
11Kigezo:ZIM1826571011987
12Kigezo:UGA171933691965
13Kigezo:CIV171833681965
14Kigezo:MAD101533581965
15Kigezo:MAR91215361973
16Kigezo:ANG9717331987
17Kigezo:LES838191991
18Bendera ya Morisi Mauritius61927521987
19Bendera ya Libya Libya6816301978
20Kigezo:NAM41015291991
21Kigezo:TAN4810221965
22Kigezo:ZAM4422301965
23Bendera ya Mali Mali447161965
24Kigezo:GAB4419271965
25Kigezo:BOT4410181991
26Kigezo:MOZ42[1]71987
27Kigezo:ERI3[1]262007
28Kigezo:SUD3[1]371973
29Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Democratic Republic of the Congo236111965
30Bendera ya Jamhuri ya Kongo Republic of the Congo[1]715231965
31Bendera ya Jamhuri ya Afrika ya Kati Central African Republic[1]2251991
32Bendera ya Guinea Guinea[1]2[1]41973
Bendera ya Sierra Leone Sierra Leone[1]2[1]41991
33Kigezo:SWZ[1]09101973
34Bendera ya Chad Chad[1]09101965
35Bendera ya Cabo Verde Cape Verde[1]0231999
36Kigezo:BUR[1]0[1]21987
37Kigezo:SOM[1]00[1]1973
38Kigezo:SEY01318311987
39Bendera ya Burkina Faso Burkina Faso037101965
40Kigezo:TOG0210121965
41Bendera ya Niger Niger02681965
42Kigezo:BEN02351973
43Bendera ya Gambia Gambia02021973
44Kigezo:RWA02021987
45Bendera ya São Tomé na Príncipe São Tomé and Príncipe0[1][1]22003
46Bendera ya Malawi Malawi00221987
47Bendera ya Guinea-Bisau Guinea-Bissau00[1][1]1999

 Ushawishi

Baada kusikia kuhusu michezo ya Pan-Afrika wakati akiwa katika ziara za kibiashara huko Kongo, mwanadiplomasia Mrusi - Muarmenia Ashot Melik-Shahnazaryan alipata wazo la kuanzisha michezo ya Pan- Armenia.

                                                                                                                                                                 


     SONG' KITANZINI                                                                                   
Alex Song
Mchezaji wa Cameroon Alex-song
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal, Alex Song, amepigwa faini na shirikisho la mchezo wa soka nchini Cameroon, kufuatia mzozo uliozuka kati yake na mshambuliaji Samuel Eto'o.


Eto'o hakupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu na kamati kuu ya nidhamu ya shirikisho hilo Fecafoot.
Mchezaji wa Tottenham Hotspurs, Benoit Assou-Ekotto naye alipewa onyo na kamati hiyo ya nidhamu.
Mashtaka dhidi ya wachezaji hao yalihusiana na mchuano wa kufuzu kwa kombe la taifa bingwa barani Afrika dhidi ya Senegal tarehe 4 mwezi Juni na pia katika kambi ya mazoezi kabla ya mechi hiyo.
Song alikataa kumsalimia Eto'o wakati wawili hao walipokutana kabla ya mechi hiyo.
Wawili hao walikuwa wametofautiana wakati fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini na mechi hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya Song tangu fainali hizo na timu hiyo ya taifa.
Song alipigwa faini ya US$2,000 na pia kuamriwa kufanya mazoezi ya siku tatu ya timu ya taifa ya vijana chipukizi mwaka ujao.
Samuel Eto'o
Samuel Eto'o

Eto'o alikabiliwa na mashtaka ya kukosa kufika kambini na pia kumdharau kocha wa timu hiyo Javier Clemente wakati mchezaji huyo alipopinga mabadiliko yaliyotekelezwa na kocha huyo.
Hata hivyo mashtaka hayo dhidi ya Eto'o yalifutiliwa mbali, baada ya uchunguzi kufanyika.
Assou-Ekotto, ambaye hakufika katika kikao cha kamati hiyo, amepewa onyo pia kwa kukosa kuitikia wito wa kufika kambini.
Timu ya Indomitable Lions inakabarua kigumu kufuzu kwa fainali za kombe la taifa bingwa barani Afrika zitakazoandaliwa nchini Equatorial Guinea na Gabon mwaka ujao.
Timu hiyo inashikilia nafasi ya tatu kundi lao alama 5 nyuma na Senegal na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
                                                                               





                                                                                                                                                                 
FACEFOOT  YAMTAKA ETO'O
                                                                                                                    
Samuel Eto'oMshambulizi matata wa Inter Milan, Samuel Eto'o na wachezaji wengine wawili, watafikishwa mbele ya kamati ya nidhamu ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Cameroon (Fecafoot).

Wachezaji hao wengine ni pamoja na Benoit Assou-Ekotto anayechezea klabu ya Tottenham na mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal, Alex Song.
Mashtaka dhidi yao yanahusiana na mechi yao ya kufuzu kwa fainali za kombe la taifa bingwa barani Afrika dhidi ya Senegal iliyochezwa tarehe 6 mwezi Juni mwaka huu na wakati walipokuwa kambini kabla ya mechi hiyo.

Eto'o ajitetea.

"Ikiwa nimesababisha matatizo yanayohusu nidhamu katika kikosi chetu cha taifa, wana uhuru wa kuniadhibu," Eto'o aliliambia televisheni ya taifa nchini Cameroon.
Eto'o anahitajika kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu kwa sababu hakushiriki katika mazoezi ya kikosi hicho, baada ya kutofautiana na Song na kuwa aliingilia kati mabadiliko ya wachezaji katika mechi yao dhidi ya Senegal.
Wakati wa mechi hiyo ambayo timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya 0-0, Eto'o alielezea kutoridhishwa kwake baada ya mshambulizi Eric Maxim Choupo-Moting alipoondolewa na mahala pake kuchukuliwa na mlinda lango Henri Bedimo.
Song naye ameamrishwa kufika mbele ya kamati hiyo kufuatia majibizano yao na Eto'o.
Alex Song
Mchezaji wa Arsenal Alex Song.


Siku chache kabla ya mechi hiyo, Song ambaye alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza na kikosi hicho, kombe la dunia mwaka uliopita, alikataa kumsalimia Eto'o mbele ya vyombo vya habari na mashabiki wa timu hiyo ya taifa.
Assou-Ekotto naye anahitajika kuelezea sababu za kutofika kambini licha ya kuwa alifahamishwa mapema.
Wachezaji hao watatu wamepewa siku nane kujibu mashtaka dhidi yao na wana uhuru wa kufika mbele ya kamati hiyo wao wenyewe, au kutuma mawakili wao.





Jiji la London litakuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka 2012 ya Olimpiki. Je London imejiandaa vipi na michuano hiyo? fuatilia maandalizi na matayarisho ya viwanja na wachezaji na kusikia uzoefu wa wachezaji katika maisha yao binafsi na pia uwanjani