MADOIDO

MATANGAZO.

ADV

AURORA MARQUEE STYLE.

23 June 2011

"MWISHO WA VITA UMEFIKA."

http://www.obama-biography.info/wp-content/uploads/2009/06/barack_obama.jpg
mwanzo wa kumaliza vita vya miaka 10 akiamuru kuondolewa kwa wanajeshi elfu 33 wa Marekani ifikapo mwishoni mwa mwaka 2012.

Katika hotuba yake jana rais Obama aliwaambia watu wa Marekani mwisho wa vita umefika.

Amesema wanajeshi elfu 10 wa mwanzo wataondolewa mwishoni mwa mwaka huu.
Wanajeshi laki moja wa marekani wanafanya kazi afghanistan.  Vita vya afghanistan vimepata umaarufu mdogo kwa umma wa Marekani huku mamilioni ya dola yakitumika katika vita hivyo nchini Afghanistan na Iraq katika muongo uliopita. Rais Obama alikiri kwamba umefika wakati wa kuzingatia zaidi kuijenga Marekani.

Rais amesema ifikapo mwaka 2014 taratibu za mpito  nchini Afghanistan zitakuwa zimekamilika kwa watu wa nchi hiyo kuchukua majukumu ya usalama nchini mwao.

Katika hotuba yake ya dakika 13 rais Obama aligusia kwamba kundi la al-Qaida liko katika shinikizo zaidi tangu shambulizi la kigaidi  la septemba 11 na karibu litashindwa. Majeshi maalumu ya Marekani yalimuuwa kiongozi wa al- Qaida Osama bin Laden huko Pakistan mei 2.

Naye mchambuzi wa masuala ya kisiasa hapa Marekani bwana Mobhare Matinyi aliyefuatilia hotuba ya bwana Obama alisema ilikuwa ya kisiasa zaidi.
Bwana matinyi alisema rais aliahidi kuondoa majeshi ya Marekani alipogombania urais na ilimbidi atimize ahadi hiyo huku akitegemea kura za wamarekani .

Bwana Mobhare pia amesema kuondoa majeshi ya Marekani huko Afghanistan kutalegeza mzigo wa deni na labda kutasaidia kuimarisha uchumi wa Marekani.

Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza

No comments:

Post a Comment