Wanajeshi wa Muungano wa Afrika nchini Somalia wameuteka mji mihumu karibu na jiji kuu Mogadishu baada ya wapiganaji wa Kiisilamu kuondoka eneo hilo. |
Mji wa Afgoye umekua ngome kuu ya kundi la Al-Shabaab ambapo wapiganaji hao wanatumia eneo hilo kuulenga mji wa Mogadishu.
Mmoja wa wakaazi wa Afgoye ameambia BBC kuwa wanajeshi wameingia mji huo na vifaru vyao vinazingira mji wote.Taharuki imetanda mji wa Afoye huku maduka yakifungwa ambapo raia wengi wameonekana kusalia nyumbani.
Wadadisi wamesema kwa kundi la Al- Shabaab kupoteza mji huo ni pigo kubwa, japo wapiganaji hao wanaaminika kujificha katika maeneo ya vichaka na mashamba ya karibu.
Afgoye ambayo huwa Kaskazini Magharibi mwa Mogadishu ni njia muhimu inayounganisha maeneo ya Kaskazini, Magharibi na Kusini mwa Somalia.
Mji huu umetumika na wapiganaji wa Al Shabaab kulenga jiji la Mogadishu licha ya kutimuliwa mji mkuu na majeshi ya Muungano wa Afrika.
No comments:
Post a Comment