Ugumu wa maisha ndiyo husababisha watu kugombana na hata kufikia hatua ya kupigana mpaka kudhalilishana. Hawa ni mafundi Uashi walipokua wamedhulumiana malipo yao ya ujira kama sehemu ya malipo baada ya kazi. Kila siku nawaasa Waafrika wenzangu kupendana, kuheshimiana, kuvumiliana na hata kuelewana, kwamfano hawa mafundi ikitokea watoto wao wanatokea hapa au wake zao, kweli heshima itakuwepo? Mimi nadhani hawa jamaa walipaswa kuelewana ili wafanye kazi kwa umoja na mwisho wa siku tuijenge AFRIKA YETU. Kirukaafrika na Afrika Yetu inawaomba vijana kuijenga Afrika kwa pamoja na si kuwekeana visasi mwisho wa siku tutajenga taifa bovu na kizazi kijacho hakitatuelewa.
|
No comments:
Post a Comment