MADOIDO

MATANGAZO.

ADV

AURORA MARQUEE STYLE.

11 July 2011

"UNA NJAA? SOMA HII"


Wazo Ngosingosi ( kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( watatu kulia) mara baada ya kuwa mtu wapili kumaliza shindano la kula chakula kilo moja ya wali,wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, za kimkoa zilizofanyika Julai saba mwaka huu eno la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga.



Washiriki 14, kati ya hao wanawake wanne, washindano la kula chakula , kilo moja ya wali, wakichuana vikali, shindano hilo maalumu liliandaliwa kwa ajili maadhimidho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara Kimkoa zilizzinduliwa Jilai Mosi na kufikia tamati Julai saba mwaka huu eneo la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga , hata hivyo tamati zake kitaifa zitafikia Desemba 9, 2011.


katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, alibuni shindano la kula ambapo alinunua mchele wa kutosha na kwa upande wa kitoweo cha nyama ya kuku , kuku walinunuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu.
Washiriki 14 walijitokeza kati ya hao wanawake walikuwa ni wanne , na ulifanyika siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya kimkoa Julai saba, mwaka huu eneo la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga na kuhudhiriwa na mamia ya wakati wa eneo hilo pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa .
Mshindi wa kwanza, Sudi Kilamilo alipatiwa sh: 35,000 na ngao , mshindi wa pili Wazo Ngosingosi , alizawadiwa sh: 25,000 na mshindi wa tatu , Omary Manjawa , kuambulia sh: 10,000.




Baadhi ya watazamaji wa shindano la kula chakula kilo moja ya wali wakiangalia sahani zilizojazwa chakula hicho kabla ya kuanza shindano hilo maalumu la Kimkoa wa Morogoro kuhusu miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara zinazotarajia kufikia tamati Desemba 9, 2011, Mkoa wa Morogoro ulipangia kuadhimisha kuanzia Julai Mosi hadi Saba mwaka huu,ambapo zilifanyika Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga.

No comments:

Post a Comment