![]() |
wafungwa wakisafirishwa |
Mwanajeshi mmoja wa Israeli Gilad Shalit, anatarajiwa kuachiliwa huru baadaye leo, baada ya kuzuiliwa kwa miaka mitano, huku wafungwa wa Palestina wapatao 1,000 wakiachiliwa huru kufuatia makubaliano na kundi la Hamas.
Hapo jana mahakama ya juu nchini Israeli ilikataa ombi la familia za waathirika wa mashambulio yaliyotekelezwa na wanamgambo wa Palestina, kutaka ubadilishanaji huo wa wafungwa ucheleweshwe kwa saa 48.
Kundi la kwanza wa wafungwa 477 wa Palestina wataachiliwa huru mapema hii leo.
Wengine wapatoa 550 wanapangiwa kuachiliwa huru mwezi ujao.
Katika barua aliyoiandika kwa familia za waathirika, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema, '' Naelewa ugumu mlionao kukubali kuwa maovu yaliyotekelezwa dhidi ya wapenzi wenu hayatalipwa kama inavyopaswa''.
Wakati huo huo mjini Gaza, kundi la Hamas linajiandaa kuwakaribisha wafungwa 295 wanaotarajiwa kupelekwa katika eneo hilo.
Waziri wa mambo ya ndani huko Gaza amewasihi wakazi ''kujizuia kutumia silaha na mabomu kuelezea furaha yao''.
No comments:
Post a Comment