Rahma Swai ambaye alikua Miss Mtwara 2011, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo mkoani Mtwara alikokua akifanya kazi Pride Radio ya mjini Mtwara secretary. Rahma ambaye kifo chake kimewastua wengi wakiwemo ndugu zake na wazazi wake waishio Dar-es-Salaam, wanasema hawajagundua kama mwanao alikua akisumbuliwa na ugonjwa wowote maana hajapata taarifa zozote mpaka hapo mwili wake utakapowasilishwa usiku wa leo ukiwa na vipimo vya kitabibu kueleza kama mwanao alikua akisumbuliwa na ugonjwa wowote. Rahma ambaye mbali na kua Miss Mtwara Pia alishiriki Miss Kanda ambapo hakufanikiwa kutwaa taji lolote zaidi ya kuwa kinara katika kinyanyiro cha Miss Mtwara na kuibuka mshindi wa kwanza. Kirukaafrika na Afrika yetu inawapa pole wale wote walioguswa na msiba huu M/Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. |
|
No comments:
Post a Comment