Mr.LOVER
LOVER Mwanamuziki Shaggy kutoka pande za Kingstone Jamaica na marekani
akiondoka kwa kucheza huku akiwa ameshikilia usinga na kusindikizwa na
vigoli wa kabila la kisukuma wakati alipokuwa akiondoka katika eneo la
tukio mara baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma, katika
tamasha la ngoma za asili la Siku ya Mavuno yaani (Bulabo) kwa Kisukuma
lililofanyika katika kijiji cha Kisesa mahali ambapo pana makumbusho ya
Bujora yaliyohifadhi tamaduni zote za kanbila la wasukuma.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Jaji Mark Bomani akimshukuru
Shaggy mara baada ya kumtawaza kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika
kijiji cha Kisesa.
Shaggy
akiwa amekalisha katika kiti cha kichifu cha kisukuma mara baada ya
kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika kijiji cha Kisesa nje
kidogo ya jiji la Mwanza, kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Lager
Allan Chonjo na anayefuata ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline
Ndungu.
Hapa naye akikabidhi baadhi ya zana kwa wafayakazi wa Serengeti Breweries baada ya kutawazwa.
Mzee
wa kabila la Kisukuma akimkabidhi mkuki mwanamuziki Shaggy wakati
alipokuwa akitawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika makumbusho
ya Bujora kijiji cha Kisesa.
Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Jaji Mark Bomani akizungumza na mwanamuziki Shaggy kabla ya kutawazwa rasmi.
Wanakijiji wa Kisesa wakicheza moja ya ngoma za kabila la wasukuma.
Chifu
Charles Kaphipa akizungumza katika tamasha hilo la Bulabo kabla ya
kumtawaza mwanamuziki Shaggy, wanaosikiliza kutoka kulia ni Chifu
Makwaiya, Allan Chonjo, Caroline Ndungu, Mwanamuziki Shaggy na Mzee
Mark Bomani.
Wanakijiji wakiwa wamefurika kwa ajili ya shughuli hiyo kubwa na inayoheshimika sana kwa kabila la wasukuma.
Mwanamuziki
Shaggy akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline Ndungu huku
wakipepewa kwa nyungo na vigoli wa kabila la wasukuma.
Mwanamuziki Shaggy akisindikiwa na Vigoli wa kabila la Kisukuma wakati akiingia katika uwanja wa ngoma za Bulabo.
Hapa
Shaggy akiwa katika jumba linalohifadhi vifaa mbalimbali vya ngoma za
wasukuma, kulia ni Padri Fabian Mhoja ambaye ndiyo mhifadhi wa
makumbusho ya Bujora (kushoto) ni Jaji Mark Bomani Mwenyekiti wa (SBL)
Shaggy akisalimiana na mzee Pius Ng'wangu wakati alipofika hapo katika makumbusho ya Bujora.
Padri
Fabian Mhoja ambaye ndiyo mhifadhi wa makumbusho ya Bujora kushoto
akimpa mwanamuziki Shaggy maelezo ya makumbusho hayo ya kabila la
wasukuma wakati, mwanamuziki huyo alipofika katika makumbusho Bujora na
kujionea mambo mbalimbali katika makumbusho hayo, katikati kutoka
kushoto ni Jaji Mark Bomani , Caroline Ndungu na Bahati Singh kutoka
Serengeti Breweriers.
No comments:
Post a Comment