MADOIDO

MATANGAZO.

ADV

AURORA MARQUEE STYLE.

27 August 2011

WOLPER NA UTAPELI MTANDAONI.


Mwigizaji mwenye mvuto Bongo Jacqueline Wolper Massawe, amedaiwa kutapeli kupitia njia ya mtandao kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook imefahamika. Akizungumza kwa hasira kupitia chombo kimoja cha habari hapa nchini Wolper alisema kuna mtu ambaye anatumia jina lake vibaya kupita mtandao huo wa Facebook kwa kuomba hela watu wakidhani ni mlimbende huo mcheza filamu kumbe sio yeye kabisa. "Nimekasirishwa sana na mtu huyo anayeliyumia jina langu vibaya na kuwachukulia hela watu ambao hudhani wanachart na mimi kumbe sivyo kabisa. Kwanini mtu atumie jina langu kujinufaisha?" Maneno hayo yalimtoka Wolper huku akimlaani mtu na kumuonya endapo akimjua ni lazima atamchukulia sheria mkononi. Kirukaafrika na Afrika Yetu, inalaani vikali kitendo cha mtu huyu anayetumia jina la mtu vbaya kwa kumchafulia jina lake na kwa mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment