Binti machachari asiyeisha skendo kunako tasnia ya Bongo Movie Elizabeth Michael (LULU) kushoto aliyemshika shati mwenziye, anasakwa na polisi jijini Daresalaam kwa kumtapeli kijana ajulikanae kwa jina la Mandela Luta "Jacob" (kulia) kwa kile kilichodaiwa kuwa ni makubaliano ya kumuandikia Script iliokwenda kwa jina la "FOOLISH AGE" ambapo Lulu na Jacob walikubalina kulipana sh. 500,000/= ambapo Lulu alimpa sh.300,000/= kama malipo ya awali. Pamoja na kumuandikia Script pia walikubaliana kuwa Jacob acheze kwenye sinema hiyo ambapo Lulu alimuahidi kumnunulia nguo za kucheza filamu hiyo, lakini baadaye ikawa ni nyuma na makubaliano yao. Baada ya Jacob kumuulizia malipo yake ya mwisho ndipo Lulu akamjia juu na kufikia hatua ya kutoleana maneno machafu na ya matusi ndipo Jacob akaamua kuchukua kila kilichochake na kuamua kuondoka kambini Lamada Hotel walipokua wameka Kambi ya Filamu hiyo. Jacob ameamua kumuchukulia RB yenye namba OB/RB/20847/11. Popote atakapopatikana ni kumuweka nguvuni. |
No comments:
Post a Comment