Zaidi ya wafungwa elfu moja nchini Kyrgistan wameshona midomo yao, kupinga hali mbaya za magereza.
Hata hivyo mamlaka za huko zinasema magenge ya uhalifu ndio yanachochea hali hiyo ili waweze kutoroka gerezani.
Kyrgistan ni nchi iliyokuwa chini ya utawala wa kisovieti, na ina wananchi milioni tano, na wafungwa elfu saba na mia sita. Kwa miaka mingi kumekuwa na matendo yanayofanywa na wafungwa, lakini hili la Jumamosi iliyopita lilizidi kiwango.
Kwanza wafungwa wengi walifanya mgomo wa siku kumi wa kula. Lakini hatua ya kuishona midomo yao imekuwa ya kipekee kiasi cha kutikisa maafisa wa magereza.
Mwandishi mmoja wa habari wa AP alishuhudia baadhi ya wafungwa wakiwa wamejishona midomo huku wakiwa wamebakiza tundu dogo tu la kupitishia maji. Wafungwa hao wametumia nyuzi ngumu na hata waya kujishona. |
No comments:
Post a Comment